283 NIMEYASIKIA MENGI

1. Nimeyasikia mengi aliyofanya Yesu
Alipokuwa hapa duniani. Pote alitenda
mema, aliwasaidia. Kwa furaha ninaimba:
”Yesu ni yeye Yule”.


Yesu ni yeye Yule Jana leo,daima!
Hutafuta wakosa, Huokoa waovu.
Mwokozi ni yeye Yule.


2. Na kipofu yule, Jina lake ni Bartimayo,
Aliposikia Yesu apita, Kwa imani akaomba
Akaponywa na Yesu. Nafurahi kwa kuimba:
”Yesu ni yeye Yule”.


3. Wenye dhambi na wagonjwa na maskini waitwa
kwa Yesu, Mwokozi mwenye rehema. Uiguse
nguo yake, sawa na mama yule, Utapewa nguvu
zake, Yesu ni yeye Yule!


4. Nasikia jinsi alivyowaombea Maadui wake
msalabani. Aliteswa kwa miiba, aliona uchungu.
Kwa furaha ninaimba: ”Yesu ni yeye Yule.”

Comments