284 TUMESOMA MENGI

1. Tumesoma mengi juu ya Bwana Yesu
Upendo wake, Ishara zake. Na usome tena,
Ukamwombe Bwana, Na utaona maajabu.


Hata leo yanatokea, Tunapoomba kwa imani.
Tuombe tu, Atusika, Na tutaona maajabu.


2. Jamaa ya Naini Wakosa amani,
Wafadhaika, Wahuzunika. Bali Bwana
Yesu ’kafanya ajabu. Aliyekufa ’kahuika.


2. Ahadi ya Mungu, Roho Mtakatifu,
Ilitimizwa Yerusalem. Walikutanika,
Roho akashuka, Kwa lugha mpya wakamsifu


3. Petro kahutubu, wengi wakatubu,
wakaghairi Dhambi za siri. Waliopokea
Neno lake Bwana Wakabatizwa siku ile.


4. Nilimwomba Yesu, Nikapata nguvu,
Na jambo hili ni la fadhili, Nilisamehewa
Dhambi zikafutwa, Nimeupokea wokovu.

Comments