1. Arusini huko Kana Yesu alialikwa,
Hapo ikaonekana Ishara ya ajabu.
Ushushe Baraka zako Ju-u ya ndugu hawa,
Bwana na Bibi-arusi. Uwaongoze vema.
2. Leo tunakuhitaji Uwe pamoja nao,
Bwana na Bibi-arusi. Ndoa ibarikiwe
3. Yesu U mlinzi wao, Uwalinde taabuni.
Uhifadhi nyumba yao, Waishi kwa amani.
4. Katika raha na taabu Wafungane kwa
pendo, Watumike kwa furaha Mpaka
siku ya mwisho.
Comments
Post a Comment