1. Mungu Baba wa mbinguni Usikie maombi,
Ndoa hii uibariki Idumu kwa amani.
:/:Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!:/:
2. Ndugu hawa mbele zako Na mbele ya Kanisa
watimize Neno lako, Wapendane daima.
3. Ndugu wawe na umoja Kwa shida na furaha,
Kama Yesu na Kanisa Wanavyounganika.
4. Bwana walinde daima, Bariki nyumba yao,
Ili waishi salama, Kwa raha na upendo.
5. Wabariki, Mungu Baba, Watu hawa wawili,
Wape upaji wa wana, Wafurahishwe kweli.
6. Siku zao duniani Zitakapotimia,
Wape urithi mbinguni, Pamoja naye Yesu.
Comments
Post a Comment