1. Tunamtia mikononi mwako Mtoto huyu ili,
Atunzwe,Na kila siku kwa neema yako,
Bwana Yesu Kristo,umbariki!
2. Ulimwenguni kuna majaribu, mahali
Pote kuna mitego, Lakini uwe Mchungaji
Wake, Na umwongoze, Ee Rafiki Mwema
3. Yesu umhifadhi kwa upendo, Asije
Akashindwa njiani, Na umlinde kwa
Rehema yako, Apate kuwa wako siku zote.
4. Utume nuru ya neema kwake, Na maji
Hai kutoka kwako, Ee Bwana Yesu
Twaku-omba leo: ”umlinde mwana wetu
Salama!”
Comments
Post a Comment