289 NINATAMANI KWENDA

1. Ninatamani kwenda mbinguni nchi yangu,
Niliyopewa na Mungu kwa imani. Ni
Shangwe bora kuona mji ule, Kwa
Kwenda kule sitaogopa kitu.


Ee Baba yangu niongoze, unisafishe kwa
damu ya Mwokozi! Nifananishwe na
theluji, Unibatize kwa Roho Mtakatifu!


2. Ee Mungu tumepata Mwana Yesu Kristo.
Kipawa kweli kinachoshinda yote.
Anahubiri amani kwao wote, walio huku
Karibu, nao mbali.


3. Kwa Yesu tumepata mwisho wa upendo
Na njia ya kumwendea Baba Mungu. Si
Wapitaji na tena si wageni, Tunatumika
Kwa roho ya upendo.


4. Amani kwetu na matumaini tele, Salamu
Toka kwa Mungu wa milele. Ni posho ya
Watumishi wa upendo Tutaurithi uzima
Wa milele.

Comments