29 BWANA U SEHEMU YANGU

  1. Bwana U sehemu yangu, Rafiki yangu Wewe. Katika safari yangu, ’tatembea na wewe. Pamoja na wewe. Pamoja na wewe, Katika safari yangu, ’tatembea na wewe.


  2. Ma’li hapa sikutaka, ili niheshimiwe, Na yanikute mateso, Sawasawa na Wewe. Pamoja na wewe, Pamoja na Wewe. Heri nikute mateso, sawasawa na wewe.


  3. Niongoze safarini, Kisha unichukue. Mlangoni mwa mbinguni, Niingie na wewe, Pamoja na wewe, pamoja na wewe. Mlangoni mwa mbinguni, Niingie na wewe.

Comments