290 BARAGUMU LITALIA SANA

1. Baragumu litalia sana, Watu wote
Watalisikia. Waliokufa watafufuka na
Wazimawatabadilika.
:/:Nani anayeweza? Yesu mwenye uwezo.:/:


2. Na wenye uwezo wa dunia Watatetemeka
Siku ile. Na hawataweza kuinuka
Kutazama uso kama jua.
:/:Nani anayeweza? Yesu mwenye uwezo.:/:


3. Najua Mchunga wangu mwema, Anichunga
Kwa maisha yangu, Na siku ya mwisho
Nikishinda, Sitaona uchungu wa kufa.
:/:Nani Mchunga mwema?Yesu Mwenye uwezo.:/:


4. Mbinguni hakitafika kitu cha uchafu,
Dhambi na kuasi. Wasiomwamini Bwana
Yesu Ghadhabu ya Mungu yawangoja.
:/:Nani atahukumu? Yesu mwenye uwezo.:/:


5. “Mimi Yesu mzabibu kweli, Baba Mungu
Ndiye mkulima, Na ninyi matawindani
Yangu, Na hamwezi neno bila mimi.”
:/:Nani ni mzabibu? Yesu mwenye uwezo.:/:


6. Unayempenda Baba Mungu Lazima
Umpende ndugu yako, Ukiwa hupendi
Ndugu yako, Huwezi kumpenda Baba Mungu.
:/:Nani aliyesema?Yesu mwenye uwezo.:/:


7. “Nawapenda mwisho wa Upendo, Na ninyi
Mpate kupendana, Hivyo mataifa
Wataona ya kwamba m-watu wangu kweli.”
:/:Nani mwenye upendo? Yesu mwenye Uwezo.:/:


8. Sisi watumishi wake Mungu, Tu watu
Maskini kati’ yote. Tutakapowekwa pa
Kuume, Kelele la sifa litashinda.
:/:Tutamsifu nani? Yesu, mwenye uwezo.:/:

Comments