291 MIMI MKOSAJI NILIKOMBOLEWA

1. Mimi mkosaji nilikombolewa, Alipojitoa
Mwokozi. Dhambi zangu zote
Alizichukua, Kwa damu nilikombolewa.


Dhambi zilitungikwa msalabani
Alipojitoa Mwokozi. Maumivu makuu!
Walimdharau, Alipobeba dhambi zangu.


2. Yesu wa upole anihurumia, Ananitakasa
Rohoni. Nimesafishwa na nimewekwa
Huru toka laana ya torati.


3. Naambatana na Yesu, siondoki, Kwa
Kuwa alinifilia. Yesu, nakusifu
Uliyenipenda, Ukachukua dhambi zangu.

Comments