292 KATIKA DAMU

1. Katika damu safi ya Yesu Dhambi zangu
Zilifutwa. Katika mto ule wa afya
Nalindwa na nguvu zake.


Nguvu za wokovu! Nguvu za ushindi!
Nazipata kisimani kinachojaa tele.
Nguvu za wokovu! Nguvu za ushindi
Damu inayonisafisha.


2. Kwa wingi wa neema ya Yesu Nimepona,
Nimepona! Wokovu ni kwa ajili yako, Na
Kwa kila ’aminiye.


3. Nguvu zangu hazitoshi kweli, Ni dhaifu,
Ni dhaifu, Ila Yesu anifahamuye,
Aniwezesha daima.


4. Baba yangu mwema anipenda, Anilinda,
Anilinda! Sitaogopa nguvu za mwovu,
Yesu yu pamoja name.

Comments