1. Shangilieni Ee watu wa Mungu! Yesu
Bwana alitumwa kwetu. Neema kubwa,
Pendo la ajabu tum-sifu Mungu siku zote!
Mungu wetu mwenye mamlaka yote
U ngao na kimbilio letu, Unayasikia
maombi yetu, jina lako litukuzwe!
2. Shangilieni Ee watu wa Mungu!
Tumwimbie nyimbo za furaha! Tusiogope
Bali tumwamini, Twende mbele kwa uwezo
Wake!
3. Shangilieni Ee watu wa Mungu!
Tumeokoka kutoka dhambi. Jirani zetu
Wasioamini, tuwaongoze wamjue Yesu!
4. Shangilieni Ee watu wa Mungu! Mfalme
Wetu yuaja tena! Kitambo kidogo tutaingia
Mbinguni kwake Mwokozi wetu!
Comments
Post a Comment