1. Dhambi zangu zimeondolewa, Mambo ya
Giza nimeyaacha. Yesu Kristo amenisafisha,
Ninamfurahia Mwokozi wangu.
Ninalo kao mbinguni Nami nimepewa
vazi, Thawabu ya ushindi ni Taji ya uzima.
Yesu ni Mwokozi wangu. Alinikomboa,
Alilipa deni langu Pendo lake kubwa nalisifu
daima, Ninamfurahia Mkombozi.
2. Nimeokoka toka gizani, Zimekwisha siku
Za huzuni. Nikapata raha na amani,
Wakati Yesu aliponikomboa.
3. Shaka na hofu zimeondoka, Na siogopi
Mauti tena. Yesu Kristo ni rafiki yangu.
Kwake ninalindwa vema siku zote.
4. Roho wa Mugu anijaliza, Ananifariji
Safarini. Yesu Kristo yu karibu nami,
Yeye ni ngao yangu na kimbilio.
Comments
Post a Comment