297 CHAKULA CHA ROHO

1. Chakula cha roho Nipe Bwana,
Ulivyogawanya mkate kale.
Bwana wangu nakutegemea.
Kwa neno uonekane kwangu.


2. Ukaja mkate Wa uzima.
Ni neno linaloniokoa.
Nipe nguvu zako, na daima
Nigawie Neno la uzima.


3. Bwana umtume Roho wako
Kuniongoza katika Neno.
Uniguse macho, niwezeshe
Kukutazama katika Neno

Comments