1. Unajua jina tulilopewa tuokolewe kwalo?
Linasifiwa duniani pote katika watu wote.
Yesu ndilo jina lipitalo Kila jina
duniani! Ni lenye nguvu ya
kutuokoa kutoka dhambi zote.
2. Linafariji moyo wa huzuni, Latutia raha kuu.
Katika shida na hatari huku Yesu ni ngome yetu.
3. Jina hilo katika giza huku hung’aa kama
Nyota.Latuliza dhoruba na mawimbi
Katika moyo wangu.
4. Majina yote yasahauliwa, Ila jina la Yesu
Milele litang’aa huko juu. Yesu jina zuri mno!
Comments
Post a Comment