3 MBINGUNI NINAYE RAFIKI

  1. Mbinguni ninaye rafiki, Ndiye mwema,
    ndiye mwema. Damu yake yanikomboa,
    Kutoka mwovu na dhambi. Asikia ombi
    daima, Ahadi ya taji anipa, Nitakayovikwa
    kwa neema, Mwendo utakapokwisha.


  2. Katika neno ninaona, Wema wake,
    Wema wake. Mnyenyekevu na mpole,
    Ni mwema kupita wote, Ashinda wote
    kwa ushujaa, Anastahili kusifiwa,
    Nikiwa naye ninashinda, Juu ya adui zangu.


  3. Amelifuta deni langu, Limefutwa,
    limefutwa. Na dhambi zangu ‘kaondoa,
    Mzigo nimepumzishwa. Sasa ninapendwa na
    Mungu, Navikwa uzuri wa Yesu,
    Kwa hiyo ninamtolea, Sifa kwa kum-tukuza.


  4. Sasa naimba kwa furaha, Kwa furaha,
    kwa furaha, Maana Mungu ameandaa,
    Mahali pa kupumzika. Hazimo huzuni na
    shida, Na kifo hakitaingia, bali uzima
    wa milele. Amani haitakwisha.


  5. Na humo namwona Mwokozi, Nimpendaye,
    Nimpendaye, Aliyemwaga damu yake,
    Kipatanisho kwa wote. Na humo wimbo
    utavuma, Moyo washikwa na furaha, Nayo
    itabakia kwangu, Hata milele mbinguni.

Comments