30 TARUMBETA LA KRISTO

  1. Tarumbeta la Kristo, Linasikika po pote,
    Na Wakristo wote wajipanga kupiga vita,
    Juu ya mahodari wa Shetani, kweli
    Twashinda.Yesu yu mbele yetu!


    Twende Yesu atuita! Twende na Wakristo
    wote! Twende na tusiogope! Yesu yu
    mbele yetu!



  2. Neno la akida kwamba tuandamane naye,
    Yeye anatutangulia, Twende mbio sote!
    Kwa silaha zake Mungu kila mtu
    ashinde. Yesu yu mbele yetu!


  3. Tukiwa mbali na akida wetu tutashindwa,
    Tutafungwa na adui na hata kupotea,
    Tukiwa karibu naye tutashinda kabisa.
    Yesu yu mbele yetu!


  4. Tarumbeta litalia na vita itakwisha,
    Na askari wote wapata matunzo na raha.
    Watapumzika na kushangilia milele,
    Yesu yu mbele yetu

Comments