300 BWANA MUNGU NASHANGAA

1. Bwana Mungu nashangaa kabisa,
Nikifikiri jinsi vilivyo. Nyota ngurumo,
Vitu vyote pia viumbwavyo kwa uwezo wako.


Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe
ulivyo mkuu. Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo Mkuu.


2. Nikitembea pote duniani,
Ndege huimba nawasikia.
Milima hupendeza macho sana,
Upepo nao nafurahia.


3. Nikikumbuka vile wewe Mungu,
Ulivyom-peleka Mwanao,
Afe azichukue dhambi zetu,
Kuyatambua ni vigumu mno.


4. Yesu mwokozi utakaporudi,
Kunichukua kwenda Mbinguni,
Itaimba sifa zako milele,
Wote wajue jinsi ulivyo.

Comments