301 WAMWENDEA YESU

1. Wamwendea Yesu kwa kusafiwa, Na kuoshwa
Kwa damu ya Yesu? Je, neema yake
Umemwagiwa? Umeoshwa kwa damu ya Yesu?


Kuoshwa kwa damu Itutakasayo
ya Yesu; Ziwe safi nguo nyeupe mno,
Umeoshwa kwa damu ya Yesu?


2. Wamwandama daima M-kombozi, Na kuoshwa
Kwa damu ya Yesu? Yako kwa M-sulubiwa
Makazi, Umeoshwa kwa damu ya Yesu?


3. Atakapokuja Bwana arusi, Uwe safi kwa damu ya
Yesu? Yafae kwenda mbinguni, mavazi Yafuliwe
Kwa damu ya Yesu.


4. Yaliyo ya takataka yatupwe, Na uoshwe kwa damu
Ya Yesu. Huoni kijito chatiririka? Na uoshwe kwa
Damu ya Yesu.

Comments