1. Eneza habari humu duniani,
Po pote panapo moyo Wa huzuni.
Ndimi za Wakristo zitangaze Neno,
Yupo Mfariji.
Yupo Mfariji, Yupo Mfariji,
Roho Mtakatifu, ndiye Msaidizi.
Eneza habari humu duniani, Yupo Mfariji.
2. Mfalme wa wafalme, Yesu,
Umtazame, Ametuletea siha ya milele;
Mateka wapate ukombozi wake,
Yupo Mfariji.
3. Niwezeje mimi kutamka vizuri,
Kumsifu Mwokozi aliye mbinguni?
Nitangaze sasa neno la furaha,
Yupo Mfariji.
4. Wenzangu, tuimbe nyimbo za milele,
Mbinguni tujaze na shukrani tele,
Upendo wa Bwana ujulike sana,
Yupo Mfariji.
Comments
Post a Comment