305 SITAISAHAU SIKU

1. Sitaisahau siku niliyobatizwa Na Roho
Mtakatifu. Nilishika ahadi, Nikaamini kweli,
Roho wa Mungu akashuka.


Na moto wa Mungu unawaka,
Hata leo moto unawaka. Bwana
Yesu atakuja kutuchukua kwake.
Na moto wa Mungu unawaka.


2. Na nguvu ya ajabu ilijaa moyoni,
Nguvu ya Roho wake. Nilijazwa imani,
Upendo, tumaini. Ni katika Roho wa Mungu.



3. Sasa nakuuliza, Je, wewe unapenda Kujazwa
Roho wake? Kumbuka Bwana Yesu,
Yeye aliahidi: Utampata Roho wa Mungu.

Comments