1. Bwana Yesu atakuja Baragumu ’talia.
Hapo wote watamwona katika utukufu.
Na tuangalie sote Mafuta ya taa zetu
Ili akija Mwokozi Tumlaki hewani.
2. Waulizwa, u tayari Kuonana na Mungu? Je,
Unampenda Yesu, Washika amri zake?
3. Tukivutwa na dunia, Na kunaswa na dhambi,
Mwisho Tutakuta giza, Na kifo cha milele.
4. Heri angojaye Yesu Na aliye tayari.
Siku moja Atapewa Tuzo ya utukufu
5. Uniongoze Mwokozi, Nifike bandarini.
Na Nitakapowasili Nipum-zike kwako.
Comments
Post a Comment