1. Giza la usiku latoweka, Nyota ya asubuhi
Yang'aa. Mapambazuko yanatangaza
Siku ya kuja kwake Yesu.
Bwana yuaja, Bwana yuaja! Shida za
dunia zitakwisha! Bibi-arusi wa
Bwana Yesu Atapokelewa mbinguni.
2. Mbele ya kiti chake cha enzi Wasimama
Watakatifu Wakimsifu Mwokozi wao Kwa
Ushindi waliopewa.
3. Yesu Bwanangu unihifadhi, Niwe tayari kila
Siku. Mbingu na nchi zikitoweka Msingi wa
Imani wadumu.
Comments
Post a Comment