310 KUNA ARUSI MBINGUNI

1. Kuna arusi Mbinguni Ndiyo ya Mwana
Kondoo. Wewe utakuwa humo Au kubaki nje?


Ndugu utakuwa wapi Milele na milele?
Rafiki ujiulize Utakuwa wapi?


2. Baragumu litalia Bwana ’taonekana
Malaika wataimba Na kumsifu Mungu.


3. Lango litafunguliwa Sifa zitavuma.
Nje itakuwa giza Hakuna furaha.


4. Ndugu utakuwa wapi? Jifikirie sana.
Mungu anapokuita Heri uitike.


Comments