315 WAKO WAPI WANAOMTII

1. Wako wapi wanaomtii Mungu Wanaoyatafuta
Mavuno? Wavune kwa haki na kwa bidii,
Wasichoke kamwe kwa kumtii.


Nani anayemfuata, Anayekubali kwenda kazini, Na
kuvuna kwa ajili Ya ghala ya mbinguni kwa furaha?


2. Ee, watu wa Mungu na twendeni Kuvuna mavuno
Ya milele! Tusimwache mtu yeyote
Tumkaribishe kwake Mwokozi!


3. Tazama mashamba yameiva, Na sasa yanangoja
Kuvunwa. Lakini wachache wanakwenda Ingawa
Maelfu wahitajiwa.


4. Ee, mtumishi mwenye moyo mkuu, Uende
Kuvuna wakati huu! Yuaja Mfalme! Vumilia!
Utafurahishwa kwake huko juu.


Comments