1.Kuomba kwafaa sana kwa watoto wa Mungu.
Wakimwomba Baba yao kwa bidii. Ahadi zake
Zote zinasimama kweli. Zimetimizwa zote katika
Yesu.
Tumwamini Mungu wetu, azijua haja zetu zote,
Hakuna neno gumu kwa Mungu aliye juu.
Kuomba kwa Mwenye haki kwafaa sana.
2. Danieli hakuacha kumwomba Mungu wake.
Ingawa alikatazwa na Mfalme. Akatupwa katika
Shimo kubwa la samba, Akaokoka kwa mkono wa
Mungu.
3. Wanafunzi wa Yesu na waliiongojea,
Ahadi ya Roho Mtakatifu. Mungu akawajaza,
Wakanena kwa lugha. Na watu elfu tatu
Waliokoka.
4. Kulikuwa na Mtu, aliyeomba-omba. Akatarajia
Kupata kitu, Petro akamwambia kweli fedha
Hatuna. Bali kwa jina la Yesu Usimame.
5. Mungu ni Yeye yule hata siku ya leo. Na maneno
Yake hayatapita, Uombe kwa imani na utaona
Kweli. Ya kwamba Mungu asikia maombi.
Comments
Post a Comment