32 KALE NILILEMEWA


1. Kale nililemewa, na mzigo wa dhambi,
Niliona rohoni, Kifo na giza tu,
Kilio na huzuni Mungu, ’kasikia,
Akaniponya na kunipandisha.


:/: Nimepona, Nimepona! Yesu Mwokozi
wangu ’kaniokoa :/:


2. Sasa Yesu ni ngome, Kimbilio langu,
Na pendo lake kubwa, Limo ndani yangu.
Neema ya ajabu Imenijaliza,
Niwe mwaminifu kwake daima.


3. Ewe, mwenye huzuni, Kuna tumaini,
Yesu anafahamu, Kukusaidia, Na
atakupandisha kutoka dhambini, Upokee
neema, Uokoke!


4. :/: Uokoke, Uokoke! Yesu Mwokozi
mwema, Akuokoe! :/:


Comments