320 BWANA MUNGU AWABARIKI

1. Bwana Mungu awabariki, Awe pamoja na ninyi,
Awalinde kwa amani! Mungu awe nanyi daima!


Mungu awe nanyi daima Hata tuonane mbinguni!
Mungu awe nanyi daima Hata tuonane huko juu!


2. Bwana Mungu na awalinde, Na kuwahifadhi vema
Kwa mikono ya rehema! Mungu awe nanyi daima!


3. Bwana awape nuru yake, Na awashibishe mema
Kwa fadhili zake Bwana! Mungu awe nanyi daima


4. Bwana Mungu awaongoze, Na wakati wa kuhama
Mpelekwe kwa salama! Mungu awe nanyi daima!


5. Mungu awe nanyi njiani, Awalinde mwe huru!
Awaangazie nuru! Mungu awe nanyi daima!


Comments