322 BWANA AMEFUFUKA

1. Bwana amefufuka Yu pamoja nasi, najua kwa
Hakika Kwamba anaishi. Naona wema wake,
Ananisikia Na safarini ananiongoza.


Yu hai! Yu hai! Yesu yu hai leo! Yu Rafiki,
Yu Mwokozi, Aliyeniokoa! Yu hai! Yu hai!
Leo anaishi! Na kama unamfikia Atakupokea.


2. Ananijali kweli Na ananilinda Kwa shida na
Furaha Tunafuatana. Najua yu pamoja Nami
Siku zote Na atatawala hata milele.


3. Enyi, watu wa Mungu, Tumwimbie sote Sifa na
Haleluya Leo na milele! Yeye ni Mfalme wetu,
Tumaini letu Na hakuna Mwokozi ila Yesu!


Comments