323 NIMETEMBELEA MBALI


1. Nimetembelea mbali, Sasa narudi. Nilipotea dhambini, Sasa narudi.


Narudi, narudi, Kutoka mbali. Sasa unikaribishe, Bwana, narudi.


2. Nimepoteza miaka mingi, Sasa narudi. Tena nazitubu dhambi, Sasa narudi.


3. Nimechoka na dhambi, Bwana, Sasa narudi. Neno lako naamini, Sasa narudi.


4. Nimevunjika, siwezi, Sasa narudi. Nipate nguvu na amani, Sasa narudi.


Comments