324 NITWAE HIVI NILIVYO

1. Nitwae hivi nilivyo, Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu, naja, naja.


2. Hivi nilivyo kipofu, Maskini na mpungufu,
Wewe u mtimilifu Bwana Yesu, naja, naja.


3. Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni;
Daima ni mashakani. Bwana Yesu, naja, naja.


4. Nawe hivi utanitwaa; Nisithubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, naja, naja.


5. Hivi nilivyo; mapenzi Yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi Bwana Yesu, naja, naja.


Comments