1. Ni wako Wewe, nimekujua, Na umeniambia;
Lakini Bwana, nataka kwako nizidi kusongea.
Bwana vuta, vuta nije nisongee, Sana,
kwako mtini. Bwana vuta, vuta nije
nisongee, Pa damu ya thamani.
2. Niweke sasa nikatumike Kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende Nizidi kukwandama.
3. Nina furaha tele kila saa Nizungumzayo kwako;
Nikuombapo, nami napata Kujua nia yako.
4. Mapenzi yako hayapimiki, Ila ng'ambo yaliko.
Anasa pia sitazijua Bali kufika kwako.
Comments
Post a Comment