1. Huru kama ndege bustanini,
Sasa nafurahi kwa sababu Yesu ni rafiki
yangu mkubwa; Nina amani daima.
2. Aliniokoa na mashaka,
Alinipa tunu ya rehema. Mimi ni mtoto
wa Babangu, Na nuru yang’aa sasa.
3. Ninataka kumshukuru Bwana,
Alitupa dhambi zangu mbali, Sitasumbuliwa
nazo kamwe, Hazinitawali tena.
4 . Jua likifichwa na mawingu,
Kiti cha rehema ni karibu, Hapo ndipo
shida ziishapo, Roho yangu yatulia.
5. Radhi kama mwana kwa babake,
Kwa salama, kama bandarini, ninapumzika
kwa Mwokozi, Mbali na shida na dhiki
6. Yesu yu karibu siku zote,
Anachukua mizigo yangu, Ninapokea
kutoka kwake, Neema na marudi pia.
7. Nilimpa Yesu moyo wangu,
Ninapenda kumtumikia, Nami
ninapenda Neno lake, Nira yake ni laini.
8. Nafurahi sana kanisani,
Kati’ ya watoto wa Babangu, Roho wa
neema ni karibu, Anifurahisha sana.
9. Mimi ni mdogo duniani,
Tena msafiri na mgeni, Kwetu ni
mbinguni huko juu, Babangu aniongoza.
10. Siku za mashaka zitakwisha,
Kuja kwake Yesu ni karibu. Nitaona raha
kubwa sana, Nyumbani mwa Baba yangu.
Comments
Post a Comment