34 KWA PENDO LAKE KUBWA


1. Kwa pendo lake kubwa, Alinitafuta,
Na alinichukua begani zizini. Na nyimbo
za malaika zikajaza mbingu pia.


Alinitafuta, akaniokoa, akanitoa matopeni,
Na kunirudisha zizini.


2. Mchunga mwema Yesu aliponya roho,
Na akaniambia: “Mtoto mpendwa!” Sauti
yake ya pendo, Ikanifariji moyo.


3. Ninakumbuka sana Damu ya Mwokozi,
Na taji ya miiba, Mateso na kifo, Na hapo
kwenye msalaba, namshukuru Yesu Bwana.


4. Napenda kumfuata Yeye nuru yangu,
Uzuri wa ahadi wanipa imani. Milele
naendelea, Kum-sifu Yesu Bwana.


5. Wakati unapita Nangojea siku,
Utakaponiita, Niende huko juu,Na nitakaa
kwa amani, Kwako, Mwokozi, mbinguni.


Comments