1. Nimefika kwa Mwokozi, sasa rohoni mwangu,
Jua lake la neema Linang’aa kila siku.
Roho yangu yaimba, Amenifungulia,
Nimemkaribisha Yesu, Naimba kwa furaha.
2. Uvumi wa neema yake, Wasikika moyoni,
Na mawimbi ya wokovu, Yajaza roho yangu.
3. Sasa Bwana Yesu Kristo, Ameingia kwangu,
Nimepewa Mfariji, Roho Mtakatifu.
4. “Siku Roho afikapo Mtajua hakika,
Kwamba ninakaa kwenu”. Ndivyo Yesu asema.
5. Kweli, amefika kwetu, Sasa yu ndani
yetu.Ujikabidhi kwa Yesu, Aoshe roho yako.
6. Yesu atakapokuja Katika utukufu,
Nitafanishwa naye, Na nitamshukuru.
7. Tutaimba kwa shangwe, Tufikapo mbinguni,
Tutashangilia kweli, Kwa kumsifu Mwokozi.
Comments
Post a Comment