36 YESU AMENIOKOA


1. Yesu amenikoa, Anipa utulivu.
Kwake ninaona raha, Napenda kumsifu.


Haleluya, Haleluya! Nimefika salama,
Haleluya, Haleluya! Kwa Mwokozi ninakaa.


2. Kwa furaha ninaimba, wimbo mpya wa sifa,
Nisichoke kamwe hapa, Kumwimbia Masiya.


3. Ni habari za neema, Za kupasha kwa bidii,
Wahubiri, mwende mbio, Pote ulimwenguni!


4. Siku nitakapokufa , Maisha yamepita,
Yesu ’nichukue kwako, kwenye raha milele!


Comments