1. Tangu siku hiyo aliponijia, Akae moyoni
mwangu, Sina giza tena ila mwanga pia,
Kwa Yesu Mwokozi wangu.
Amani moyoni mwangu, Kwa Yesu
Mwokozi wangu, Sina shaka kamwe kwa
sababu Yeye, Yu nami moyoni mwangu.
2. Sina haja tena ya kutanga-tanga, ndiye
kiongozi wangu. Dhambi zangu zote
zimeondolewa, na Yesu mwanawe Mungu.
3. Matumaini yangu ni ya hakika, Katika
Mwokozi wangu. Hofu zangu na hamu
zimeondoka, Kwa kuwa ninaye Yesu.
4. Nitaketi na Yeye huko milele, Nisifu
Mwokozi wangu, Nina raha moyoni majira
yote, Kwa Yesu Mwanawe Mungu.
Comments
Post a Comment