1. Nilikwenda mbali sana Katika njia
mbaya, Nikamsahau Yesu Aliyenifilia.
Nina raha na furaha, Yesu ’kanitafuta,
Akaniokoa kweli, Mimi wake daima.
2. Na sikufikiri siku Nitakaposimama,
Mbele ya Mwenyenzi Mungu, Ili nihukumiwe.
3. Dhambi zilinichokesha Nikarudi kwa Mungu,
Akasema neno zuri, La kufariji moyo.
Comments
Post a Comment