Skip to main content
- Usiku kabla ya kuteswa Yesu,
aliwakusanya wanafunzi, Alifahamu
kwamba saa yake,Ya kutolewa inakaribia
- Kwa roho aliona Gethsemane,
Mateso yake, huzuni nyingi, Zaidi alihofu
saa ile, Atakapoachwa hata na Mungu.
- Alitamani saa ya Pasaka, Pamoja
nao wapendwa wake. Katika pendo lake
kubwa sana, Aliyashinda majaribu yote.
- Akautwaa mkate, aka’mega: “Twaeni, mle,
mwili wangu huu.” Na akawapa
wanafunzi wake.Yu heri kila mtu ’aminiye.
- Baadaye akawapa na kikombe, akasema:
“Nyweni nyote hiki! Ni damu yangu
inayomwagika, Kwa ondoleo la makosa yote.”
Comments
Post a Comment