1. Watu wa Mungu, mshangilieni kabisa,
Na Mwimbieni Mfalme wa mbinguni na nchi.
Yupo Nasi kwa pendo kubwa kweli Ili tupate wokovu.
2. Ona ajabu! Mwokozi aliyejidhili! Pendo kamili
Na neema nyingi ya Mungu. Akafanywa kuwa
Ni mwanadamu Atukomboe dhambini.
3. Sisi Wakristo, tumwimbie sote pamoja Yesu
Mwokozi aliye dhabihu ya kweli! Atukuzwe
Hapa na juu mbinguni, Kwani alitufilia!
4. Yesu Mfalme, Kwa pendo uliniokoa Nikufuate,
Nitakutumikie daima! Juu mbinguni Nitakusifu
Tena kati ya watakatifu.
Comments
Post a Comment