1. Muda mwingi nilipotea, Sikufahamu
msalaba,Wala aliyenifilia, Msalabani
Rehema bure na neema, Samaha nalo
nilipewa, Ndipo aliponifungua Msalabani.
2. Kwa neno lake Bwana Mungu, Nilijiona mimi
mwovu, Nikageuka na kutubu, Msalabani.
3. Yote nam-tolea Yesu, ndiye Mfalme wa pekee
sasa. Kwa furaha nitamwimbia, Bwana Yesu.
4. Jinsi pendo lilivyo kuu, Neema ilishushwa toka
juu. Alitufanyia wokovu Msalabani.
Comments
Post a Comment