42 BWANA YESU AMEVUNJA


1. Bwana Yesu amevunja, Minyororo Ya dhambi,
Nimewekwa huru kweli, Asifiwe Mwokozi!


Haleluya, Haleluya! Yesu Kristo Mwokozi!
Haleluya, Haleluya! Yesu ni Mkombozi.


2. Nilipoungama dhambi, Nikapewa uhuru,
Moyo wangu unawaka, Kwa furaha na pendo


3. Kamba zilizonifunga Yesu amezitoa.
Dhambi zilizosumbua Zimefutwa kabisa.


4. Nataka kushuhudia: “Nimepewa uhuru”.
Kwa furaha nipeleke, Neno zuri la Yesu.


Comments