1. Juu ya mwamba lajengwa,
Kanisa lako tukufu, Limewekwa huru
kweli, Katika damu ya Yesu.
Juu ya mwamba, Limejengwa kanisa la
Yesu Kristo, Juu ya mwamba, Juu ya
mwamba, Tutasimama imara.
2. Nimepewa neema kuu,
Kuwa pamoja na Yesu. Vita yangu
imekwisha, Nimejazwa utulivu.
3. Katika nyumba ya Mungu,
Nimekuwa jiwe hai, Kama kiungo cha
Kristo, Nashiriki mwili wake.
4. Juu ya msingi imara, Kanisa
liko salama, Na vyote vikitoweka,
Litasimama daima.
Comments
Post a Comment