44 TU WATU WENYE UHURU


1. Tu watu wenye uhuru Kwa damu ya Yesu,
Twahubiri Neno lake, Kwa moto wa Roho.
Tusichoke kwenda mbele, Tushinde majaribu!
Tuvumilie katika vita ya imani!


2. Tu wanajeshi wa Mungu, Silaha ni zake Yesu
Kristo, jemedari, Anatuongoza, Kwa nguvu yake
twashinda, Twadumu hata kufa, Na tuendelee
mbele! Tumsifu Mungu!


3. Kwa Yesu tuna ushujaa, Na mam-laka kuu,
Maana twayaamini Maneno ya Mungu. Kisima
cha m-salaba, Kiko wazi kwa wote. Maji yake
tunakunywa Maji ya uzima.


4. Mbinguni, nchi ya raha, Amani na haki.
Tutakapofika huko, Tutamsifu Yesu, Machozi
atayafuta,Yesu Mwokozi wetu. Kwa shangwe
tutaurithi, Ufalme wa Mungu.


Comments