1. Waisraeli walikaa Babeli utumwani.
Sayuni walikumbuka. Kwa huzuni nyingi.
Amri ilitolewa, Walipewa uhuru,
Mioyoni walijaa shangwe. Walipiga vinubi,
Wakaimba njiani Hata nchi ya ahadi.
2. Vinubi hawakupiga Kwa hali ya utumwa.
Hawakuweza kuimba Nyimbo za Sayuni.
3. Walipotoka Babeli, Ikawa kama ndoto,
Maana walirejea Nchi ya Kanaani.
4. Mataifa walisema: “Mungu amefanyaje?
Watumwa wanaondoka, Wamewekwa
huru!”
5. Dunia kama Babeli, Ina wafungwa wengi,
Kwa njia ya Injili tu, Watafunguliwa.
6. Amri imetolewa, Tumepewa uhuru,Shangwe kuu
mioyoni mwetu!Twende sote mbinguni, Na
tuimbe njiani,Tumefunguliwa kweli!
Comments
Post a Comment