46 SIHITAJI KUJISUMBUKIA


1. Sihitaji kujisumbukia, Mambo yatakayotokea,
Yote yamo mikononi mwake, Baba yangu
anipendaye, Yeye mwenye moyo wa upendo,
Ananipa yanayonifaa, Kama sikitiko au
shangwe, Masumbuo ama furaha.


2. Siku zote yu karibu nami, Ananipatia
neema,Yeye aitwaye Mungu Baba, Achukua
masikitiko. Kunitunza hivyo kila siku, Jambo
hilo amejitwika. Nguvu ya kunitosha daima,
Ni ahadi niliyopewa.


3. Mungu unisaidie tena, Kutulia karibu nawe, Na
kuliamini Neno lako, Nguvu yako nisipoteze!
Na katika mambo yote huku Nipokee kutoka
kwako, Nguvu na neema ya kutosha,
Mpaka nimefika mbinguni!


Comments