48 MIMI SIWEZI KUIFAHAMU


1. Mimi siwezi kuifahamu, Neema ya
Mungu kwangu, Zamani nilikuwa na
dhambi, Sasa nimesamehewa.


Bali namjua Mungu, Anayeweza kunilindia
Urithi wangu bora, Hata siku ya Yesu.


2. Mimi siwezi kulifahamu, Pendo lake la
ajabu,Ninapoamini Neno lake, Ninayo raha
moyoni.


3. Siwezi kufahamu kazi ya Roho wake
Ndani yetu, Anayeweza kutufundisha,
Kumtegemea Yesu.


4. Idadi ya siku zangu hapa, Siwezi
kuifahamu, Wala kama nitakutana na
taabu ama furaha.


5. Sijui nitam-laki Yesu, Kabla ya
kuona kifo, Ama nitachukuliwa juu,
Nikitoka kaburini.


Comments