1. Njia yote naongozwa Kwa mkono wa Yesu.
Nionapo wema wake, Sitahofu lo lote.
Nina raha ya mbinguni, Ninakaa salama.
:/: Ananitendea mema, Katika mambo yote:/:
2. Njia yote naongozwa Naye Yesu, Mwokozi.
Anilinda jaribuni, Tena nguvu anipa. Nikichoka
safarini, Na kusikia kiu,
:/: Mwamba uliopanuka, Maji yatoka kwako :/:
3. Njia yote naongozwa, Kwa upendo wake mkuu,
Atanituliza tena, Kwa Babake huko juu,
Miguuni pake Yesu, Ninam-sujudia.
:/:Nitamsifu Bwana Yesu, Kwa uongozi wake.:/:
Comments
Post a Comment