5 DHAHABU NA FEDHA

  1. Dhahabu na fedha haziniokoi,
    Mali haziwezi kuponya roho,
    Lakini kwa damu ya Yesu Mwokozi,
    Nimenunuliwa niwekwe huru.


    Nakombolewa kwa damu yake,
    Naokoka kwa neema,
    Damu yake ni ya thamani,
    Kalipa deni langu.



  2. Dhahabu na fedha hazinilipii,
    Madeni yangu ninayo kwa Mungu,
    Mwokozi alini-komboa kwa damu,
    Nipate wokovu, niache dhambi.


  3. Dhahabu na fedha haziufungui,
    Mlango wa kumkaribia Bwana,
    Lakini kwa damu nimeifikia,
    Neema ya Mungu aliye mkuu.


  4. Dhahabu na fedha hazinifikishi,
    Nyumbani kwa Mungu niliyemwasi,
    Lakini nimekombolewa kwa damu,
    Kwa hiyo nitachukuliwa kwake.

Comments