50 SITASUMBUKA KWANI MUNGU


1. Sitasumbuka kwani Mungu, Ananitunza daima,
Mizigo yangu achukua Nyakati zote za mwendo.


Siku nyingine sijaona, Na jana imetoweka,
Na leo Mungu azijua, Hitaji zote ninazo.


2. Sitasumbuka kwani Mungu, Ni Baba yangu
kabisa, Hawezi kunisahau la! Ingawa haonekani.


3. Sitasumbuka kwani Mungu, Anishibisha neema.
Anipa vitu vyote vyema, Kwa roho yangu na mwili.


4. Maua yote ayavika, Na ndege wote wa anga,
Chakula chao wapokea, Pasipo shamba na ghala.


5. Katika Bwana nafurahi, Na kama ndege naimba,
Najua kwamba kila siku, Babangu ananitunza.


Comments