1. Jua la moyo wa kila Mkristo Ni Yesu
Naona amani Golgotha Alipojitoa Yesu
:/:Na huko nina kimbilio kwa Yesu Anipendaye.:/:
2. Sitaki ‘tamani fahari Na dhambi ulimwenguni
:/:Sababu wokovu ninao Katika damu yaYesu.:/:
3. Aliindoa kabisa Mizigo ya dhambi zangu.
:/:Na niliokoka hakika Kwa neno la Baba Mungu.:/:
4. Chakula cha rohoni mwetu Ni neno la Baba Mungu.
:/:Kinamletea Mkristo, Nguvu kwa safari Yake.:/:
5. Mimi ni hekalu la Roho, Anamiliki moyoni
:/:Kwa njia ya ahadi zake Yesu ananiongoza.:/:
6. Uliye dhambini ufike Kwa Yesu Mwokozi wako!
:/:Anakunyoshea mikono apenda kukupokea:/:
Comments
Post a Comment